Unapokuwa unatamka nchi za Jumuiya ya
Madola moja kwa moja kichwani mwako, ufahamu unaingia ndani yako ni kwamba
unamaanisha nchi zilizotawaliwa au zilizokuwa koloni la Uingereza. Leo tunaendesha
magari upande wa kushoto kwa sababu aliyekuwa anatutawala alitwambia tuendeshe
kushoto. Yako mambo mengi ambayo tuliyarithi na mpaka sasa bado hatuyajabadilisha
kwa sababu tu ya yule aliyekuwa anatutawala. Matumizi ya maneno kama “District
Commissioner” “Regional Commissioner” n.k, yote tumeyarithi kutoka kwa waliokuwa
wanatutawala. Lakini pamoja na hayo kuna mambo ambayo ningeliyaita “kufanywa ndondocha
(brain washed) kuna nyimbo tulizokuwa tunaimbishwa ili kuweza kumuenzi na
kumsifu aliyekuwa anatutawala, kwa tafsiri isiyokuwa rasmi kutoka katika lugha
ya Kiingereza yalisema,” Tawala Uingereza! Tawala mawimbi yote Tawala!
Uingereza! Na wala usiwe mtumwa!” Na nyingine zilikuwa za kumuombea Malkia, “Mungu
mwokoe Malkia wetu! Mpe ushindi Malkia aendelee kututawala milele, na maneno
mengine. Tutawale sisi watumwa wako! Tutawale! Haya maneno yalikuwa yanaimbwa
kutoka katika mioyo yetu tena kwa kumaanisha! kilichokuwa kinaimbwa au kujengwa
ndani ni hiki: Kwamba tutaendelea kutawaliwa yumkini mpaka Yesu atakapokuwa
anarudi mara ya pili! Nyimbo hizi zenye maneno mazito zilikuwa zinatudumaza tusiwe
na mawazo ya kwamba sisi tunaweza kujitawala au tunaweza kuongoza! Haya
yalikuwa maneno ambayo ni ya kutufanya tusijione ya kuwa ndani yetu tanacho
kitu cha kutufanya tujitawale na kuwa huru! Maneno kama haya ni kudumaza
ufahamu wetu.
Na kwa nyimbo hizi, wale waliokuwa wanatutawala
hawakuweza kufanya “mentoring” ya kutuandaa tuweze kuwa viongozi bora! Na mpaka
leo unapokuwa unaangalia hasa matatizo tuliyokuwa nayo ilikuwa ni shida ya au
iliyotokana na kuwa “brain washed”. Leo nchi za Afrika zimejitawala kisiasa,
lakini si kiuchumi wala kijamii! Leo mipango karibu yote ya Serikali za Afrika
inategemea mawazo ya wale waliotutawala! Japokuwa viongozi wetu hawaimbi zile
nyimbo tulizoimbishwa wakati wa kutawaliwa, lakini katika eneo la kiuchumi na
kijamii bado tunaimba hizo nyimbo japo si kwa kutoa sauti!
Unapozungumzia Soko Huria- ni ukweli
usiopingika ya kuwa tunaimba nyimbo za,”Tawala Milele juu yetu!” Tawala milele
na wala usitawaliwe, wewe unayetutawala! Utawasikia viongozi wetu wakituambia
juu ya maelekezo wanayopokea toka World Bank, IMF n.k. Lakini pamoja na kutuamrisha
tunayopaswa kutekeleza, bado viongozi wa Ulaya wanawalaumu viongozi wetu kwa
utawala na uongozi mbovu, wakati kiuhalisi hawakuwaandaa! Utawala huo wa
ukandamizaji wa kikoloni haukuandaa, kuibua, kuchochea na kujenga watu ambao
wangelikuja kurithi nafasi ambazo wangeliziacha baada ya sisi kujitawala! La
ajabu hata wale wanaoitwa Americans Indians na Negro-slaves-pamoja na kwamba
wako katika nchi kama Marekani, Unakuta wana matatizo ya uongozi katika jamii
zao wenyewe! Tatizo ni nini? Waliimbishwa nyimbo za kutawaliwa na kuongozwa
bila kujua ya kuwa na wao wanao uwezo wa kufanya vyema.
UFANYE NINI? Kwa
nyimbo tulizoimbishwa na “kufanya ndodocha” (kuwa ‘brain washed) - ndani yako
ni lazima kuingia shauku ya kuchukia nyimbo hizo za “nilizaliwa kutawaliwa na
kuendelea kuwa mtumwa” Na wakati baba zetu na babu zetu wakiimbishwa nyimbo
hizo hawakujua ya kuwa zilikuwa zinawanyonga kisaikolojia! Ni lazima uwaze
kugundua ya kuwa haukuzaliwa kutawaliwa na kuwa mtu anayefuata (follower) tu
mambo ya walioko! Kwa kusema hivyo simaanishi hawatakuwepo viongozi, watakuwepo! Ila ujione ya kuwa katika gari gurudumu
haliwezi kuwa taa ya treki na usukani hauwezi kuwa kioo cha mbele maana yake,
kila kimoja ya vifaa hivyo kila kimoja ni “kiongozi-katika eneo lake na nafasi
yake haiwezi kushikwa na kifaa kingine! Rejeta ina uwezo ambao hauwezi
kupatikana katika betri ya gari!
Uongozi wa kweli haubebi tu watu
wanaowafuata bali huzalisha viongozi (True leadership does not maintain
followers but produces leaders)-Nikwambie na kukuhakikishia ya kuwa, Hakuna
anayeweza kufuta kulichomo ndani yako! Yawezekana una maswali haya!
QUESTIONS FROM THE HEART
Is leadership about power, position,
talent, skill, authority, some unique physical trait, social status, family
heritage, or special charisma? Is leadership a corporate appointment or the
reward bestowed after a struggle with competitive forces? Is leadership
reserved for just an elite few chosen by providence and separated from the
masses of us normal mortals who struggle for a sense of significance?
Does leadership require followers? Is
it necessary for leaders to have tittles? Is leadership a distinction of
superiority, a disposition of advantage and qualities of greatness that one from
the rest? s leadership a manifestation of superior intellect or cognitive
capacity? Is leadership reserved only to a specific race or class of people?
Are leaders smarter, wiser, better, greater, move intelligent, more equipped,
more skillful, and more charismatic than followers are?
These are the questions may be you
have been struggled with for some years back!
Hakuna linalotokea bila uongozi.
Hakuna linalobadilika bila uongozi .Hakuna linaloendelea bila uongozi. Hakuna
linaloboreka bila uongozi .Hakuna linalorekebishwa bila uongozi. Kila mmoja,
kila mahali, kila wakati kuna kuongozwa! Hali zozote, mazingira yoyote na namna
zozote ambazo mtu, familia, jamii, shirika, taifa ambako wanaweza kujikuta
wamefikia, ujue kuna aliyewaongoza mpaka wakawa hapo walipo! Iwe ni katika hali
nzuri au mbaya!
Mara zote iwe ni moja kwa moja au si
moja kwa moja, kutaka au kutokutaka tunajikuta tunaongozwa! kwa namna fulani
kuna anayekuwa anatuongoza ama mwanasiasa, askofu, baba, bosi au mwalimu. Hata kibofu
anaweza kuongeza kwa mujibu wa kauri ya Yes Kristo! Alisema, “Kipofu
akimwongoza kipofu mwenzake, wote watatumbukia shimoni”
Ki ukweli, tuna watu wanaotungoza
ambao tumeamua tuwe chini yao watuongoze iwe kwa kupiga kura, au kuteuliwa na
hata kwa makubaliano! Kwa changamoto tulizokuwa nazo katika karne ya 21,
Ulimwengu umejikuta unapambana na mambo kama ugaidi, vita, majanga, tabia nchi,
umoja wa wala rushwa, n.k! Changamoto ni kwamba tutapataje viongozi wa kutufaa
kuyakabili au kuja na suluhisho la kutatua matatizo kama ya uhamiaji na mambo
ya uchumi. Nchi zilizokuwa za Kisovieti kwa sasa zinahangaika kupata viongozi
watakaotatua suala la uzalishaji kibiashara pamoja na uhalifu! Afrika
tunatamani kupata viongozi watakaomaliza utamaduni wa rushwa na vita vya
wenyewe kwa wenyewe na matatizo sugu ya ukame, njaa pamoja na UKIMWI. Mataifa
yanayopitia mabadiliko ya kisiasa kama Iraq na wao wanatamani wawe na viongozi
wa kutatua yanayowakuta.
TUNA VIONGOZI WENGI, UONGOZI KIDOGO! Si
kwamba hatuna viongozi wanaoshikilia ofisi za uongozi katika jamii zetu! Tunao
viongozi wengi sana! Lakini si uongozi mwingi! Tuna viongozi katika jamii, dini,
kisiasa, na maeneo mengine, lakini viongozi hawa na waliowatangulia wamezalisha
mambo yanayokosa majibu!
Ulimwengu tunaoukaa unakabiliwa na
mambo yetu ambayo hayana budi kupatiwa ufumbuzi. Mtanziko uliokuweko leo na kwamba mengi kama siyo yote ya matatizo
tuliyokuwa nayo yamezalishwa na viongozi au na wao wameelemewa na matatizo
waliyoyarithi toka kwa waliowatangulia ! Na kila tatizo baya ni matokeo ya
uongozi dhaifu.
MFANO: Teknolojia tuliyo nayo
imeziacha tamaduni nyingine nyuma! Ni karibu 10% tu ya idadi ya watu
ulimwenguni wanaonufaika na teknolojia na teknolojia hiyo hawezi kuboresha wala
kuokoa maisha ya wengi. Maana yake pamoja na mabadiliko hayo na yanayokuja kwa
haraka hayajaweza kumeza wala kutatua katika maisha ya afya za watu!
*Jambo lingine ni ule mgawanyo sawa wa
rasilimali zetu.
Kiuhalisia, Duniani hakuna njaa! Njaa
iliyopo imetokana na matatizo ya uongozi ambao umeshindwa kupeleka mahitaji kwa
wahitaji!
Wakati fulani mtu mmoja alikuwa Marekani
na akawa anaendeshwa na mwenyeji wake kuelekea eneo lijulikanalo Fargo, North Dakota.
Wakiwa njiani akamuonyesha shamba kubwa la mahindi lililokuwa tayari kwa kuvunwa.
Lakini akamwambia, wakulima hawako tayari kuvuna mpaka bei itakapokuwa imepanda!
Na isipopanda, watayang’oa na kuyaharibu na kuyazika udongoni ili waweze kuleta
uhaba wa chakula!
Sasa kama wanaamua hayo, Je, hawajui
ya kuwa walipaswa kuyapakia mahindi hayo yaletwe Zambia, Malawi, Botswana,
Ethiopia, Somalia, Sudan ya Kusini na Kaskazini mwa Kenya ambako kuna ukame?
Lakini kwa sababu bei iko chini, North Dakota watayaharibu mahindi hayo badala
ya kuyapakia katika meli yaje Afrika.
*Wakati
mwingine chakula cha msaada kinaweza kuletwa, tatizo likawa la Usambazaji
wa kuwafikia wenye uhitaji. Nchi nyingine misaada hiyo viongozi wataihifadhi
kwa ajili yao wenyewe: Kiukweli, Hakuna umasikini ulimwenguni! Ila kuna siasa,
biashara na” viongozi wawekezaji “ambao wanashawishiwa na agenda zao wenyewe
(mfano, Guinea ya Ikweta-mtoto wa Rais Nguema, anauza madini nje ya utajiri
mkubwa wakati watu wana hali mbaya ya chakula! Ametajwa kuwa bilionea lakini
anawaibia walio wengi!)
*Jambo lingine ni suala la afya. Utafiti
unaonyesha ya kuwa, kila sekunde sitini, kuna watu 7 wanaoambukizwa UKIMWI. Na
viongozi wa afya wamekosa majibu ya utatuzi wa hilo na wanawaza watalikabili
vipi?
*Kuna suala la Kidini na mgongoni wa tamaduni. Hivi karibuni Uingereza walikuwa na mjadala
mkali, wafanyeje kwa jamii ya Waislamu waliokuwa wanapanga kuishambulia nchi
ambayo imewapokea na kuwapa raia. Unapokuwa na watu ambao ni raia, lakini
wakageuka kuwa magaidi kwa sababu ya tofauti za ki-imani, ujue kuna tatizo la
uongozi kitaifa!
*Kadhalika, Ufaransa walikuwa wanahaha kwa ongezeko la Waislamu kutoka Utarudi. Walikuwa
wanaona wabadilishe mfumo wa elimu ili kuweza kuchukuliana na utamaduni wa
uvaaji wa Kiislamu na lugha yao .Mpaka sasa viongozi hawajui wanafanyaje na
mfumo huo wa Elimu kwa sababu hata misingi ya Idara ya Uhamiaji inaonekana
kutikiswa!
*Marekani
haijaachwa nyuma! Wao nao shida imekuwa uhamiaji haramu toka Mexico. Wako
katika mahali ama waganga kutua mkubwa na mrefu kudhibiti uhamiaji haramu!
Wakati huo huo viongozi wa Congress wanaendelea kupambana wao kwa wao katika
vikao ili kupokea heshima na faida zaidi.
*Mtafaruku katika familia na wenyewe
ni tatizo lingine! 51% ya watoto katika Marekani na jamii za Magharibi,
madarasa yamejaa watoto wanaotoka nyumba zisizokuwa na baba! Unapokuwa
unapeleka watoto wa aina hii shuleni, utakuta hali inakuwa mbaya na tete
shuleni! Kwa sababu hawajui maana yake nini kutii mamlaka! Ni kwa sababu
wanapungukiwa uongozi wa wazazi wawili wanaokaa pamoja!
*Tatizo la ndoa .Tuna shida katika
uongozi kwa sababu kama viongozi wameshindwa kuja na tafsiri ya kwamba
tunaposema ndoa, je ,ni kwa ya mume na mke au
inaweza pia kuwa mume na mume au mke ana mke!
(Elton JOHN -Amefunga ndoa ya jinsia
moja na huyu ndiye tungelimwita “Muelimishaji wa jamii” na David Beckham alihudhuria!)
Leo tuna viongozi ambao sasa wanakuja
na kuhoji ni kwanini mtu asiwe na uhuru wake wa kuamua, kufunga ndoa na mnyama!
Msamiati unaoitwa” Familia”-kwa sasa uko katika mdahalo! Na sasa kama Mashoga/Wasagaji
–wataasili mtoto (adoption), hiyo ni taswira ya kuwa uongozi una shida! Maana
kama waliamua kuoana mume na mume, mke na mke inakuaje leo waasili mtoto?
Kwa sababu ya matatizo hayo ya ambayo
viongozi wetu kwa sasa wamekuwa na
hofu ya ugaidi, mgawanyiko wa jamii,
majanga, vita, magonjwa, kuanguka kwa uchumi! Na huu ndiyo Ulimwengu tunaoukaa.
Haya yamezalisha mambo yafuatayo,
KUKATA TAMAA-Kijana
anawaza! Kwa nini nisubiri kumaliza shule wakati naweza kuuza dawa za kulevya
nikapata fedha! Wazee wamekosa msimamo! Kwanini nisidanganye katika fomu ya
kulipa kodi au tu nituze heshima yangu kwa kusema ukweli?
HASIRA: Watu
wana hasira kwa kushindwa kukabili maisha ya kila siku! Watoto wana hasira na
wazazi na hata jamii inayowazunguka! Hasira hiyo imewapelekea kuingia katika
maisha yaliyoharibika na matendo mafu!
KUTOKUAMINIANA:
Kutokuaminiana na ya hali hofu ni jambo linalokua kwa haraka sana. Watu
wanakata tamaa na kuvunjika moyo kwa ahadi zisizotimizwa na serikali zao, uongo
na udanganyifu katika biashara, kukosekana kwa uaminifu shuleni, n.k.
KISINGIZIO (Compromise)
Watu waliopoteza imani kwa viongozi wao na wana uchungu, wako tayari kupoteza
uadilifu wao na mwenendo wao. Wako tayari kulala na bosi ili apandishwe cheo au
kulala na mwalimu ili apate maksi nzuri, Wako tayari kumwibia mwajiri kama
wanaona kuwa hawalipi vizuri.
UBINAFSI: Viongozi
wamekuwa wabinafsi kwa kujiangalia wenyewe! Hawajali tena watu wanaowazunguka
Hata wale walio wahitaji na wao wanajiangalia wenyewe!
mawakili nao wako tayari kuorodhesha
mashtaka lukuki ukidhani wanakusaidia kumbe wanataka kulipwa zaidi.
MASHINDANO:
Watu wanaamini raslimali ni chache kwa hiyo wanazishindania badala ya
kushirikiana
UROHO/KUTOKURIDHIKA: Kwa sababu ya matangazo watu wanatamani vitu wasivyo na uwezo navyo! kama
kijana hana uwezo kwa kununua raba ya Nike, yuko tayari kumkaba mtu kwenye kona
na kuichukua .Mtu hana uwezo wa kununua gari sawa na la mfanyakazi mwenzake
alilonalo, yuko tayari atumie karo/ada ya mwanae kununua gari hilo ili na yeye
awe katika fasten. Wazazi hawana uwezo wa kununua “Flat Screen”-wako tayari
kwenda “Tunakopesha ili waipate.
THAMANI YA UHAI IMEONDOKA: Ni kisheria, kutoa mimba na kutupa kama unaona hali fulani
haziruhusu kwa mimba uliyopata bila kutarajia! Haki za wanyama na haki ya kutoa
mimba ni mambo yenye uwiano sawa kwa sasa!
“ABUSE”: Wazazi
wanapiga watoto kwa kuwatesa, wanaume wanapiga wake zao! kwa sababu wanazojua wao.
Mwanamke anajiona hana thamani kwa mumewe na anaendelea kujiona hana thamani
hata kwa wanaomzunguka!
UHALIFU/VIOLENCE: Mauaji ya kutisha (tar 7 Januari jambazi amekamatwa na risasi 6082 na
AK 47 na SMG) Ujambazi na uporaji uliobobea, unaendelea sehemu ambazo
zinaonekana serikali yote inakaa hapo, wakati tungelidhani kungelikuwa salama
kuliko sehemu yoyote ile mauaji yaendelea, Washington D.C, Pretoria, London,
n.k.
VITA: Kuna vita nyumbani, kati ya
baba na mama, watoto na wazazi, vita shuleni kati ya walimu na wanafunzi, vita
katika biashara kati ya Meneja na waajiriwa, vita makanisani kati ya waumini na
mchungaji, vita kati ya dini na dini (mfano Boko Haram huko Nigeria) na imani
zingine ,vita kati ya taifa na taifa! wasio na hatia ndiyo washiriki wakubwa!
Yote haya katika Historia na hata leo ni
matokeo ya uongozi. Hali tuliyo nayo katika Ulimwengu ngazi za taifa na jamii
zetu ni uthibitisho tosha ya kuwa ubora na mwenendo wa uongozi wa binadamu kwa
karne nyingi haujatoa majibu ya kuridhisha!
Lakini viongozi hawa wanatoka katikati
yetu! Mila na tamaduni zetu hazizalishi viongozi wanaoweza kuweka mambo sawa! Neno
linatwambia, Kila kitu kinazaa kwa jinsi yake! Hauwezi kuzalisha kilicho bora
zaidi ya ulivyo! (You cannot produce something better than yourself) Ndio maana
viongozi tunaondelea kuwazalisha au kuwapata kwa vizazi vyote hawawezi
kuboresha wala kuleta hali bora zaidi
Kila mtu anataka kuwa viongozi
Bado watu wanataka kuwa viongozi
wanasiasa, watu wa kawaida, wanariadha (msanii wa muziki wa Senegal anayemiliki
runinga na magazeti anataka kugombea uraisi) wafanyabiashara, wanafunzi,
wanataka kuwa viongozi.
NANI MWENYE UWEZO
“The value in each human is the gift
they were born to deliver to humanity
Gari linaaminika kuwa na vifaa
vilivyoiunganisha 60,000
Lakini unaonaje ungelikosa waya
unaokuwa unaunganisha toka katika terminal ya battery”
kwenda katika Ivyine ambao thamani
yake ni shilingi 50,000/= kwa gari yangu thamani ya milioni themanini .Battery’
thamani yake ni kati ya sh. 100,000/= mpaka 150,000/= je, ukiondoa waya huo wa
elfu 50,000/= kuna madhara katika gari?
Ninachotaka kusema ni kwamba katika
gari kila kimoja kina jina tofauti na kila kimoja ndani yake kina uwezo tofauti
na kingine kwa maneno mengine kila kimoja kina uwezo tofauti na kila kingine.
Katika gari unaposema jina la kitu unakuwa unataka kuonyesha uwezo wake ambao
ni tofauti na kitu kingine kwa lugha nyingine kila kimoja ni “In charge” katika
eneo lake.
kama vifaa vinavyounda gari
vingelikuwa vinatoa taarifa kwa anayekuja kuendesha, mfano
‘Battery” iseme niko tayari!
“Plug” Iseme nina moto
“vingine” niko tayari kuendesha gari
lote! Halafu waya unaounganisha katika betri unyamaze!
Wewe ni kiongozi. Una uwezo ndani
yako!
Thamani ya wadhifa haiku katika
ukubwa au udogo wake; Bali, kwa kazi unayokuwa unaifanya!
Thamani yako iko katika kipawa
kilichoko ndani yako!
BORN TO LOAD, PROPARED TO SERVE
Wewe ni kiongozi. Ndani yako kuna
uwezo wa kuongoza. Japo katika kila tamaduni, tuna maneno unayoweza kuwa
unaaminishwa kama tulivyoona katika utangulizi ya kuwa babu zetu wake kuwa
"levain washed”- kujiona ya kuwa waliumbwa kutawaliwa na Uingereza nay a
kwamba maadamu ndani ya kila mtu kuna shauku ya kuwa kiongozi basi ni jukumu la
kila mtu kugundua, kuchochea na kutumikia kipawa au uwezo uliomo ndani yake kwa
kuwatumikia watu wengine.
Uongozi ni nini? (Jambo la kwanza ni
kutumikia Kiongozi ni mtumishi wa watu. Unafikia hatua ya kuwa kiongozi ni kwa kutambua
the god has deposited in you” na uanze mkubwa kunafikiwa pale mtu anapokuwa
ametumikia watu wengine!
Popote kipawa chako kilipo katika maisha,
si kwa ajili yako kukihifadhi, ni kwa ajili yako kukitoa kihudumie ulimwengu unaokuzunguka!
Uongozi unaotumikia wengine ni uongozi wa kujisambaza katika kizazi chake!
Distributing yourself
Usisubiri uwe na nafasi ya juu ndiyo
uanze kutumikia watu wengine, usisubiri upate digrii, usisubiri upandishwe
cheo!
Safisha vyoo na kutumika! Andaa chai
a kutumika! Panga viti na kutumika! Imba kwaya na kutumika! Tumika katika kila
fursa inapopatikana!
Servant leadership is being PREPARED
to serve your gift at every opportunity?
Kama unataka kuwa mkubwa, haina budi
kuanza kutumia kipawa chako kuwatumikia wengine bila kutaka kulipwa! (Work to
learn, not to warn). Tangulia kujitolea kwa kuwa chini ya mwingine kabla ya
kutanguliza kulipwa.
KWANINI UONGOZE?
(Never underestimate the power of
one-self)
Kwa hali isiyoridhisha ya mambo
niliyo kutajia hapo juu, tunahitaji viongozi ambao wameandaliwa kwa kujitolea
kuwatumikia!
Vyombo vya habari kila wakati
vinatwambia nchi Fulani unafanya uchaguzi, lakini unakuwa uchaguzi ambao wale
waliopiga kura wanajikuta katika wakati mgumu baada a ahadi walizopewa
kutotimizwa!
Tunahitaji watu wa kutuwezesha
nyakati ngumu. Katika Biblia tunawaona watu kama Musa, Joshua, Nehemia, Esther,
Debora, Daudi, Daniel.
Lakini hatuwezi kuwasahau akina
Teddy-Roosevelt, John F. Kennedy, Sir Winston Churchill Martin Luther King Jr, Mahatma
Gandhi, Nelson Mandela!
NB. Naamini ya kuwa matatizo katika ulimwengu
au yanaweza kutatuliwa, ikiwa kila moja atatumikia kipawa kilichomo ndani yake
kwa watu.
NI NANI ALIYE MKUBWA?
“NI YULE ATUMIKAYE”
“Everyone came to earth with
something humanity needs”
Hawa wanatajwa kutumikia badala ya
kutoka ukubwa: Mother Theresa, N.Mandela, Abraham Lincoln, Martin Luther,
Martin Luther King Jr, Michael Jordan, Tiger Woods, George Washington, Thomas
Edison, Benjamin Franklin, M. Ghandllie, Henry ford,
Bill Gates, Oprah Winfrey, Wright
Brothers, na wengine.
Somo toka Kapernaumu
Mk.9:33-35
Lk 22:24
Mt. 20:20-21---------Mt. 20:26-27
The idea is that leadership has
nothing to do with ruling people. It has more to do with year gift-identifying
it, maximizing it, and serving that gift to the world.
Baraka Edom
baraka.edom@yahoo.com
No comments:
Post a Comment