Neno kutoka Yohana 1:1 – 4
“1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno,
naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye alikuwa Mungu. 2. Huyo mwanzo alikuwako kwa
Mungu. 3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote
kilichofanyika. 4. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru
ya watu. (5. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza)”
-
Watu wengi wanakumbwa na mateso, maumivu na mahangaiko
maishani mwao kutokana na kwamba Mungu hayuko katika masiha yao. Mambo hayo
magumu yote yatakwisha mara tu mtu akitambua uwepo wa Mungu, kwani vitu VYOTE
VILIFANYIKA KWA HUYO; WALA PASIPO YEYE HAKIKUFANYIKA CHO CHOTE KILICHOFANYIKA!
-
Neno alikuja kwa walio wake, wala walio wake
hawakumtambua (laiti kama wangelitambua uwepo wake...!)
-
Kama mtu ukitambua uwepo wa Mungu kwenye maisha yako,
utampa nafasi na kipaumbele pamoja na kumwamini katika mambo yote. Na ndiyo
maana kitu kikubwa anachokifanya Ibilisi kwa watu ni kushika ufahamu wao ili
wasitambue kabisa uwepo wa Mungu, kwani anajua wakiutambua, hana lake!
Katika kitabu cha Yohana sura ya
11, ndugu zake Lazaro walitambua kuwa kama Yesu rafiki yake angalikuwapo, basi
Lazaro hangalikufa na ndivyo Martha dada wa Lazaro alivyomwambia Yesu (katika mstari
wa 21). Hii inaonesha Martha alitambua kuwa katika uwepo wa Mungu, YOTE
YANAWEZEKANA! Yesu alithibitisha nguvu za Mungu kwa kumwamsha Lazaro kutoka
usingizi wa kifo, kwa sababu kwa Mungu vyote vinawezekana, na akiwepo katika
maisha ya mwanadamu, YOTE YANAWEZEKANA
-
Kumbuka kuwa, PASIPO YEYE HAKIKUFANYIKA CHOCHOTE. Na
hata Yesu amesema kuwa “Ninyi pasipo mimi hamwezi lolote” kwa hivyo njia pakee
ya kuweza ni katika uwepo wake! Nayaweza yote katika Yeye anitiaye nguvu
-
Unaweza kujitahidi na kujiona kuwa na mafanikio katika
maisha, lakini pasipo Yeye ni kazi bure.
Tunajua wazi kuwa giza haliwezi
kuishinda nuru. Sehemu pekee giza linapotamalaki ni pale ambayo chanzo cha
mwanga/nuru kimezuiwa. Kama ukizima taa kwa mfano, kutakuwa na giza. Lakini mara
tu uwashapo taa, giza hutoweka mara moja.
Kama nuru imeweza kulishinda giza,
wala giza halikuiweza, hivyo basi kama ukiwa na Mfalme wa Nuru basi ufalme wa
giza hauwezi kukushinda. Kama ungekuwa na Yesu, mambo yote hayo magumu
unayoyapitia usingeyapitia. Uweza, mamlaka na nguvu alizonazo Mungu si za kawaida,
hashindwi na lolote lile. Nuru ingalikuwapo, giza lisingalikuwapo.
-
Shetani anatambua uwepo wa Mungu na hivyo pia kwa
matatizo. Matatizo pia yanatambua nguvu za Mungu, na kwa kuwepo na Mungu katika
maisha yako, matatizo hayatakuwa na sababu ya kuendelea kubaki, kwani katika
uwepo wake hayawezi kuvumilia kukaa
-
Yesu ndiye ufufuo na uzima, ukiamini utauona utukufu
wa Bwana (kumbuka alivyowaambia ndugu za Lazaro).
-
Hata kama matatizo yako yamechukua muda mrefu kiasi
gani katika masiha yako, ukifikia hatua ya kutambua nuru inalishinda giza,
uponyaji wako umefika tayari
-
Hata katika masomo yako, GPA yako pia itarekebishwa na
ataishibisha! Unapaswa kutambua uwepo wa Mungu katika mfumo mzima wa maisha
yako ya sasa na ya baadae. Hatupaswi kuishi tunavyoishi, bali kama vile Yeye
alivyoishi. Ukifikia kuutambua uwepo wa Mungu, shetani hawezi lolote. Palipo na
nuru giza halikai.
Mfano mmoja ni kuwa dada mmoja
alikuwa karibu kuahirisha masomo yake ya chuo kutokana na masaibu yalikuwa
yakimkuta. Alikuwa hawezi kusoma, akiingia darasani hamu yote inamtoweka. Lakini
alipopata taarifa ya kuwa Mungu kupitia mtumishi wake amewezesha wengine, akaamini
kuwa inawezekana na yeye kufanikishwa. Ilikuwa zimebaki siku mbili kabla ya
mitihani kuanza, na alikwa haelewi afanye nini.
Nilimwambia dada huyo kuwa mimi
niwe katika nafasi yake, naye awe katika nafasi yangu. Kitu nilichomuomba Mungu
juu ya dada Yule ni kuwa “ninaomba ujuzi wa maswali yote, niwe na uwezo zaidi
ya maswali na maswali yawe chini ya uwezo wangu, Amen” Hivyo tu! Dada alifurahishwa
na maombi hayo na akapata nguvu za kusoma toka siku hiyo usiku mzima hadi siku
iliyofuatia. Akaweza hata kusoma na mwenzake kamasehemu ya maandalizi ya
mitihani.
Siku ya kwanza ya mtihani maswali
aliyokutana nayo ni yaleyale ya sehemu alizozisoma. Alifurahi mno na hata
kushindwa jina la kumuita Mungu (niliomba Roho wa Mungu amsaidie) kwani
hatimaye yasiyowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu yamewezekana. Baada ya
kumaliza mitihani vizuri akiwa na furaha na tumaini la mafanikio, aliuniuliza
nifanyaje? Japo alikuwa mkristo wa madhehebu ya kiadventista, nilichomwambia ni
kuwa ampe Yesu maisha yake.
Kupitia dada huyo ninamshukuru
Mungu kwamba zaidi ya watu 30 wamevutwa kwa Mungu kwani yeye na familia yake
walikuwa wakitoa machapisho kuelezea ushuhuda wao. Kwa sasa kitabu kinaandaliwa
cha mkusanyiko wa shuhuda kinaitwa “MUNGU YUPO, NA NI HALISI”
-
Maneno ya kawaida na tuliyozoea kuyatumia, laity kama
tungejua nguvu iliyoko ndani yake, basi tusingekumbwa na masaibu na taabu
katika maisha. Mfano ni “Bwana Yesu Asifiwe”,
“Mungu akubariki” na mengineyo linapotajwa jina la Yesu uwepo wake hujaa.
Tatizo ni kuwa hatutambui uwepo wa Mungu
-
Tatizo linalotokea kwako sasa usiwe na presha, kumbuka
kama giza linavyotoweka taa ikiwashwa, ndivyo litakavyotoweka ukitambua uwepo
wa Mungu. Kama mvua ishukavyo toka mbinguni,
-
Musa alitambua uwepo wa Mungu ndiyo maana pamoja na
kuzungukwa na hatari pande zote (jeshi la Farao nyuma, mbele bahari ya shamu na
pembeni jangwa) bado aliwatia moyo wana wa Israel kuwa wasiogope, watulie na
watauona mkono wa Bwana. Na Mungu kwa nguvu zake aliwaokoa na kuliangamiza
kabisa jeshi la Farao.
-
Zakayo pia alitaka sana kumuona Yesu kwa kutambua
uwezo wake hata akapanda juu ya mkuyu, lakini Yesu alipomfikia alimwambia shuka
mtini wokovu umefika kwako, na Zakayo alishuka na kumkaribisha nyumbani kwake. Kwa
sababu ya uwepo wa Mungu katika maisha yake, aliwarudishia mara nne wale wote
aliowadhulumu.
-
Neno la Mungu halitarudi bure, bali litatimiza mapenzi
yake Yeye aliye juu
By Pastor
Covenant
Email:
covenantpastor@ymail.com