Saturday 2 February 2013

ISIKUPITE - By Preacher Regan Daud


MHUBIRI 3:4A NA C yaani wakati wa kulia na wakati wa kuomboleza, huu si wakatu mtu angependa kuufikia naandika hapa kwasababu katika wwakati huu watu wamepata shida sana na kumwacha MUNGU na wngine kudhubutu kusema MUNGU hayupo na kugeukia miungu yao. swali ni je unatambua uko wakati gani na wakati huo wa kulia ulipofika ulifanyaje/utafanyaje? uliujua na ulimtafakari nani? haya ni maswali ya msingi sana na hasa swali la je wakati wa kulia ukifika utautambua? watu wengine wanafikiria ukiokoka wakati huu huufikii ila nataka nikwambia kukaa sawa na MUNGU wako katika wakati huu ndo wakati kama usipokaa vizuri shetani atakupa shida! n atakuondoa kwenye uwepo wa MUNGU na kuchukua kibali chako. wakati YESU anafundisha anasema sikuja kuleta amani bali mtu kumfarakanisha na ndugu yake. hii inamaana mwanzo wa kuokoka ni mwanzo wa kuteseka lakini mateso matakatifu ila kama Daniel alivyosema kwamba aliadhimu moyoni mwake na wewe inakupasa kuadhimu sasa.
NDUGU yangu wakati huu ni wakati mbaya sana ambao umejaa machungu, huzuni, maumivu, na mambo yote uyajuayo mabaya lakini unapaswa uyapitie hapo napo MUNGU anakupitisha kwa utukufu wake. mojawapo ya mafundisho ya MUNGU kukupitisha huko anataka wewe umtafakari yeye sawasawa na uchukue hatua kwa ajili ya utukufu wake.
ukitambua kwamba uko kwenye wakati huo husimwache MUNGU wako ni wakati anataka uwe karibu naye zaidi. mtafakari AYUBU. husimwache BWANA MUNGU WAKO . Hebu mnene kwa ujasili. alafu utaona mkono wake. UBARIKIWE.
From: https://www.facebook.com/regan.daud

No comments:

Post a Comment