Sunday 5 October 2014

ULIMWENGU WA GIZA

Uchawi ni kazi inayofanyika kwa usiri mkubwa sana, endapo mchawi atatoa siri za wachawi wenzake adhabu yake huwa ni kifo. Ni vigumu sana kumtambua mchawi, licha ya baadhi ya makabila kuwashuku akina mama wazee wenye macho mekundu kuwa ndio wachawi, lakini ukweli siyo wachawi. Madhalani mkeo/mumeo anaweza akawa mchawi wa kutupwa lakini usiweze kumtambua kabisa. Kawaida matayarisho ya kwenda kuwanga huanza jioni ya saa kumi na mbili hadi saa mbili usiku, kwa kuchoma ubani na kuomba dua, wachawi wanayo roho ya uchawi ndani yao, ambayo ikifika saa sita usiku, hiyo roho ya uchawi iliyo ndani yake humwamsha. Wachawi wanakuwa na madhabahu zao za kukutanikia usiku, kwa mfano wachawi wa Kariakoo wanayo madhabahu yao, wachawi wa Masaki wanayo madhabahu yao, Wachawi wa Mwananyamala madhabahu yao iko ndani ya hospitali ya Mwananyamala, ndiyo maana vitimbi ndani ya hospitali hiyo haviwezi kwisha bila ya kuivunja na kuisambaratisha hiyo madhabahu. Mchawi anapoamka usiku wa manane huenda kwenye madhabahu yao, na kila madhabahu ina mwenyekiti na katibu wa kuandika taarifa za kikao. Kazi ya kikao ni kupokea mashitaka kutoka kwa wajumbe, kuyajadili na kuyafanyia maamuzi. Kwa mfano, mchawi anaweza kuleta shitaka kuwa jirani yake XYZ kila siku wanakaanga nyama na samaki, watoto wake wanasoma shule nzuri, na wanaringa sana. Hilo ni shitaka tosha la kujadiliwa kwenye madhabahu za wachawi. Wachawi wakimaliza kumjadili ndungu XYZ, wanapanga adhabu ya kumwadabisha, adhabu inaweza kuwa, wamtupie mume jini afukuzwe kazi, au wampindishe mama miguu asiweze kutembea. Wakishachagua adhabu, huteua kamati ya utekelezaji ambayo, itahakikisha familia hiyo inaadhibiwa haraka iwezekanavyo. Idadi ya wajumbe inategemea ukubwa wa kazi, lakini mara nyingi huwa ni wachawi kati ya watatu hadi sita. Wachawi huanza kazi ya ulozi nyumbani kwako, kwa kawaida muda wa kufanya ulozi ni kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa usiku, kama siku hiyo hawakufanikiwa kuingia hadi saa tisa usiku, shughuli huairishwa hadi siku inayofuata, roho ya uchawi waliyo nayo huwafanya wachawi kupenya kwenye ukuta, kwa kupitia kwenye kona ya chumba. Wachawi wakikuta mtuhumiwa ni mcha Mungu mzuri huwa wanashindwa kumkaribia kwani mwili wake huwa unawaka moto, wakikuta familia yote haishikiki, basi kikao hungeuza adhabu kwenda kwa mfanyakazi wa ndani, biashara yako, au kwa ndungu zako wa karibu. Wachawi wakikuta familia iko tupu, kazi ya ulozi huwa ni nyepesi sana, na matokeo yake huonekana mapema Majini ndio mtaji mkubwa wa wachawi/ waganga wa kishnzi katika kutimiza kazi zao za kishetani. Majini yanakuwa ndani ya mwili wa wachawi, pia wachawi wanaweza kufuga majini yao ndani ya mwili wa mtu mwingine bila mtu huyo kujijua, vipo viashiria vya wazi kabisa vinavyoonyesha kuwa ndugu/mtoto/rafiki/ mke/mume wamegeuzwa banda la kufungia majini. Kiumbe chochote chenye uhai, ili kipate kuishi ni lazima kipate chakula na maji, vinginevyo uhai wa hicho kiumbe huwa katika matatizo na hakiwezi kuishi. Wachawi wa nchi wakikufanya banda la kufugia majini, hulazimika kutafuta chakula cha kuwalishia majini yao kila siku. Chakula cha majini mara nyingi ni nyama za wanadamu na kinywaji chao ni damu za wanadamu, kawaida wachawi wote huwa wanamiliki misukule, misukule muda wao wa kuishi ukifika hufariki dunia, huko msukuleni hazikwi mtu, bali nyama yao ndiyo hutumika kulishia misukule walio hai na kulishia majini yao. Kama wachawi wamekufanya banda la kufugia majini yao, usiku huja nyumbani kwako na nyama za watu pamoja na damu, na unalishwa nyama hiyo kichawi bila wewe kutambua. Kama unashirikiana chumba kama mke na mume na ikifika usiku huwa unasikia mume/ mke anatafuna chakula kwa muda mrefu, na kitendo hicho kinajirudia mara kwa mara, ujue kuwa mwenzako analishwa chakula cha kichawi na wachawi. Ukiwasha taa huwezi kuwaona wala hicho chakula hutakiona, isipokuwa asubuhi, huyo mtu aliyelishwa chakula usiku anakuwa ameshiba kabisa na hawezi kula kifungua kinywa cha asubuhi, na mdomoni atasikia harufu ya nyama. Madhara yake baada ya muda ni mabaya sana, kwani haya majini husababisha mtu kupooza mwili mzima au upande wa mwili. Fanya uchunguzi kwa watu 50 waliopooza, utakuta watu 30 walikuwa wanatafuna vitu wasivyovijua usiku. Majini hayauzwi, isipokuwa unapoingia kwenye taaluma hii ya uchawi, ukimaliza mafunzo unapewa majini kama zana za kufanyia kazi, kumbuka kuwa kuna aina nyingi sana za majini na uwezo wao hutofautina sana. Kadri unavyomiliki majini ya kila fani ndivyo unavyokuwa maarufu katika fani hii ya ulozi. Picha Ya Wachawi walio kamatwa huko mkoani Mwanza baada ya ungo wao kudondoka. Shiriki 1 Hakuna maoni:

No comments:

Post a Comment