Monday 24 November 2014

DODOMA CAMPAS NIGHT CHAPTER IV 2014-2015



SHALOOM
Mpendwa msomaji leo nakuletea shuhuda ya PASTOR CASEN from ZAMBIA.
ALIYEHUBIRI katika mkesha wa  DODOMA NIGHT CAMPAS-INUKENI ENYI MALANGO...........

(PASTOR CASEN aliyeshika kidevu)
Katika maisha yake amefanya kila baya ambalo ni chukizo kwa MUNGU,, alipokuwa kijana mdogo wa miaka 10's alianza kunywa POMBE huku akiichanganya na SUKARI kwenye kikombe. Siku zilivyozidi sogea akaanza tumia kiliba kizima yaan lita moja ya CHIBUKU na kuendelea. hatimaye akawa mlevi wa kutupa.
Kwa kuwa alikosa upendo wa wazazi wake walipotengana akiwa mdogo sana alianza kutafuta watu mbadala wa kuchukua nafasi ya upendo wa wazazi wake na si mwingine ila girl friend. Awal aliamini mahusiano hayo yatakuwa ya barua tu, baadae wakaendelea kutembea mita moja bila hata kugusana kwa kuwa alichohitaji ni kutiwa moyo tu.. kwa kuwa kawaida huzaa desturi mara wakaanza kushkana mikono, mara kula pamoja mwishowe wakadondoka dhambini.

Baada ya mahusiano hayo yaliyotawaliwa na dhambi kuvunjika akaanza kutafuta mabinti tofauti kukidhi haja za moyo wake kwani ufahamu na akili yake ilikamatwa na pepo la UZINZI. Mtaani alijulikana kwa kuwa na kila msichana kimahusiano.

Kama ilivyo desturi kwa mtu achovyaye kumaliza buyu la asali baba huyu alianza kuvuta SIGARA kama SM, punde si punde akaanza tumia BANGE.

Akiwa na mahusiano na mke aliyemuoa alishawa kushirikiana na mkewe kutoa MIMBA nne za mkewe kabla ya kuoana

Tisa kumi, alipoanza kwenda disco alikuwa mtazamaji tu, lakini ghafla akaanza kutikisa mguu akienda disco, ghafla akaanza kuingia kwenye mashndano ya wacheza disco huko ZAMBIA.

SIKU MOJA AKIWA UKUMBI WA STAREHE akizungukwa na kila aina ya uasi AKASIKIA SAUTI YA MUNGU AKISEMA "UKIENDELEA HIVI UTAKUFA, SASA NIFUATE UITANGAZE INJILI" Kwa sasa pastor huyu ni mtumishi mkubwa wa MUNGU wa ndani na nje ya nchi. Hata mm blogger nimemuona akihubiri katika DODOMA CAMPAS NIGHT IV.

sikiliza msomaji wa makala hii, ukianza kumruhusu ibilisi katika uchache jua pia atajitukuza kwako katika wingi....biblia inasema usimpe ibilisi nafasi kabisa kwa kuwa akiingia kwako anaua, anaiba na kunyonga.
 JAMANI SISI TU MVUKE MUDA WOWOTE UNAYEYUKA TUTUBU......YAKOBO 4:13-14



No comments:

Post a Comment